Baba wa kiungo wa Simba, Jonas Mkude
amezikwa leo katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Gerrard Mkude amezikwa leo kwa ushirikiano
mkubwa wa ndugu, jamaa na marafiki waliojitokeza leo.
Msiba huo ulikuwa Kinondoni Studio nyumbani
kwa marehemu ambapo ibada ilifanyika kabla ya kwenda makaburini.
Uongozi wa Simba uliwakilishwa na Makamu wa
Rais wa klabu hiyo, Geofrey Nyange ‘Kaburu huku upande wa wachezaji
wakiwakilishwa na Abdi Banda na kwa makocha alikuwepo Kocha Msaidizi, Selemani
Matola.
Mashabiki kadhaa, majirani na marafiki wa
familia ya Mkude walijitokeza kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment