Kocha Mathias Lule ameendelea kukinoa kikosi chake cha Stand United akiwa jijini Dar es Salaam.
Stand United wameendelea na mazoezi kwenye
Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.
Lule amesema ni sehemu ya kujiandaa na
mchezo wao dhidi ya Azam FC, Jumamosi.
“Tunaendelea na mazoezi kwa ajili ya mechi
yetu dhidi ya Azam FC. Tunarajia mchezo mgumu, hivyo tunazidi kujiandaa,”
alisema.
Licha ya kufungwa na Yanga kwa mabao 3-2 mechi iliyopita, wachezaji wa Stand walionekana wakiendelea na mazoezi vizuri kabisa.
Baadhi yao wamesema wamepania kushinda ili
ikiwezekana warejee nyumbani kwao Shinyanga angalau wakiwa na pointi mkononi.
Licha ya kupoteza katika mechi dhidi ya Yanga, vijana wa Stand United walionyesha soka safi na la kuvutia hivyo kuwapa wakati mgumu Yanga.
0 COMMENTS:
Post a Comment