Vinara wa Ligi Kuu bara, Yanga wameendelea
na mazoezi yao leo kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar.
Yanga wameendelea na mazoezi kujiwinda kwa
ajili ya mechi yao dhidi ya Ruvu Shooting itakayopigwa kesho.
Pamoja na kufanya mazoezi ya kukimbia, Hans
van der Pluijm aliwaongoza vijana wake kucheza soka la haraka huku akisisitiza
kila upande kutopoteza mpira.
Uchezaji wa kila kikosi ulionyesha kuwa
makini huku kila upande ukitaka kushinda dhidi ya mwingine.
0 COMMENTS:
Post a Comment