Wakati bondia wa ngumi za kulipwa Mtanzania, Mohammed Matumla
akishindwa kupata majibu ya kama atakwenda kuzichapa nchini Marekani au la,
taarifa rasmi zinaonyesha nafasi hiyo amepewa bondia kutoka Morocco, Said El
Harrack.
Licha ya ushindi dhidi ya Mchina, Wang Xin Hua, lakini promota
aliyesimamia pambano la Matumla na Mchina, Jay Msangi, amesema safari ya
Matumla imeshindikana kwa kuwa ameshindwa kufikia vigezo vilivyowekwa na
waandaji wa pambano la Manny Pacquiao dhidi ya Floyd Mayweather.
“Suala la Matumla kwenda Marekani ilikuwa ni moja ya ahadi zetu
iwapo atashinda na tulituma mkanda wa video kwa meneja wa Pacquiao ambaye ndiye
ameupeleka kwa waandaaji ambao wao wanaamini kwamba Matumla hawezi kupigana
siku hiyo kwa kuwa hakufikia vigezo wanavyotaka wao.
“Sababu kubwa waliyoitoa wao ni kwamba Matumla alishindwa katika
mapambano yake mawili ya nyuma, pia katika pambano dhidi ya Mchina alicheza
faulo nyingi, sasa wao wameona ni vema nafasi hiyo apewe huyo Mmorocco kwa
sababu ameweza kukidhi vigezo,” alisema Jay Msangi.
0 COMMENTS:
Post a Comment