Mmoja wa wanachama maarufu wa Coastal Union,
Nassor Bin Slum amesema ni wakati mwafaka kwa wanachama wa klabu hiyo kurudi
pamoja na kuungana.
Bin Slum ameshauri wanachama wasahau tofauti
zao, waungane kwa lengo la kuisaidia klabu hiyo na timu yake lakini ukifika
wakati wa uchaguzi wa viongozi wajue kuwa uchaguzi huo ni muhimu sana kwa
maisha ya klabu yao.
“Ukifika wakati huo wa uchaguzi, basi wachague
viongozi sahihi ambao wataiongoza Coastal Union katika njia sahihi.
“Wawe viongozi ambao wataiondoa Coastal katika
makundi na wawe wanaotaka kuifanya Coastal ni moja,” alisema Bin Slum na
kuongeza.
“Kwa sasa tunaungana kwa kuhakikisha timu
inabaki katika ligi kuu. Baada ya ligi, unafuatia uchaguzi na lazima mashabiki
wawe makini sana.
“Tukubaliane kuwa kuna sehemu tulikosea,
Coastal Union ilikuwa na makundi na ndiyo yaliyochangia matatizo makubwa
yaliyojitokeza.”
Bin Slum aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa
Coastal Union, pia mdhamini wa klabu hiyo.
Lakini ilitokea hali ya kutoelewana na uongozi
wa klabu hiyo hadi walipomuomba kurejea asaidie baada ya mambo kuwazidi nguvu
na hawakuwa na ujanja tena.
Ingawa wengi walitarajia kumuona Bin Slum
akikataa kurejea, yeye aliwashangaza wengi kurudi kuisaidia Coastal Union
akisisitiza ni klabu anayoipenda tokea utoto na yuko tayari kusaidiana na
wengine kuisaidia.
0 COMMENTS:
Post a Comment