Mshambuliaji Emmanuel Okwi ya Simba, ametoa
yake ya moyoni kuhusiana na kikosi chake kuwa na mwendo wa kuyumba.
Okwi raia wa Uganda amefunga mabao matatu, hat
trick na kuisaidia Simba kuiadhibu Mgambo Shooting kwa mabao 4-0 katika mechi
ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Akizungumza na SALEHJEMBE baada ya mchezo huo,
Okwi aliwataka mashabiki kuendelea kuwaunga mkono ili washinde zaidi kwa kuwa
si nia yao kupoteza.
“Kweli matokeo yetu yamekuwa si mazuri, hatuna
mwendo mzuri lakini inakuwa si nia yetu kucheza katika kiwango cha chini.
“Tunapenda kufunga na kushinda kila mechi,
mashabiki wasichoke kutuunga mkono wakati tunaendelea kupambana,” alisema.
Okwi amesema bado hawajakata tamaa kuendelea
kuitafuta nafasi ya pili katika Ligi Kuu Bara.
Ushindi wa leo dhidi ya Mgambo umeiwezesha
Simba kulipa kisasi cha kufungwa na Mgambo katika mechi ya kwanza lakini
imejiongezea pointi tatu na kufikisha 38.
0 COMMENTS:
Post a Comment