Mashabiki wa Simba Ukawa wamefariki dunia katika ajali mbaya ya gari
iliyotkea leo jioni nje kidogo ya mji wa Morogoro.
Mashabiki wanne wa Simba Ukawa wamefariki dunia na watu wengine
wawili walioelezwa kuwa ni abiria pia wamepoteza maisha.
Taarifa kutoka katika eneo la ajali zimeeleza mashabiki hao walikuwa
njiani kwenda mjini Shinyanga kuishangilia Simba inayopambana na Kagera Sugar
kwenye Uwanja wa Kambarage.
Imeelezwa gari hilo aina ya Toyota Coaster limeacha njia ghafla na
kuingia porini kabla ya kuanguka.
Baadhi ya majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Morogoro
nab ado wanapata matibabu huku mmoja wao akiwa taabani.












0 COMMENTS:
Post a Comment