![]() |
| BASI WALILOKODI NA KULILINDA, HALAFU HAWAKULIPANDA.... |
Yanga wameonyesha wamekomaa baada ya kung’amua mchezo mchafu waliokuwa wamefanyiwa na FC Platnum.
Dakika baada ya kutua kwenye Uwanja wa Ndege Joshua Nkomo mjini Bulawayo,
Zimbabwe, Yanga walikwenda kupanda basi la mashabiki.
Kilichowashangaza wahusika wa FC Platnum ni kuona wachezaji wa Yanga
wakipanda basi lililotua mjini hapa likiwa na mashabiki kutoka jijini Dar es
Salaam.
Tayari viongozi wa Yanga waliotangulia mjini hapa walikodi basi
ambalo lilikuwa linalindwa muda wote.
![]() |
| BASI WALILOPANGIWA NA KULIKATAA.... |
Hata baada ya kutua kwa Yanga, hawakupanda basi hilo badala yake
wakapanda lile la mashabiki aina ya Toyota Coasta ‘Mayai’.
Mashabiki nao wakapanda katika basi lililoletwa uwanjani na uongozi
wa FC Platnum kwa ajili ya kuipokea Yanga.
Dereva wa basi lililoletwa na Platnum alikuwa akilalama kwamba
alitumwa kubeba wachezaji na si mashabiki. Lakini haikusaidia.










0 COMMENTS:
Post a Comment