Taifa Stars imepangwa kuanza na Uganda katika
mechi za kuwania kucheza michuano ya Kombe la Mataifa Afrika kwa wachezaji
wanaocheza ndani (Chan).
Ratiba ya Shirikisho la Soka Afrika (Caf)
iliyopangwa leo mjini Misri, mechi ya kwanza itakuwa kati Juni 19 hadi 21 na
kurudiana kati ya Julai 3 hadi 5.
Iwapo Stars itafanikiwa kuing’oa Uganda, basi
moja kwa moja itakutana na Sudan ambayo imefuzu automatically katika raundi ya
kwanza.
Mara ya kwanza na mwisho, Stars ilishiriki
michuano ya Chan mwaka 2009 baada ya kuing’oa Sudan.
Michuano hiyo ilifanyika nchini Ivory Coast na
Stars ilishindwa kusonga hadi hatua ya robo fainali baada ya sare ya bao 1-1
dhidi ya Zambia katika mechi iiyopigwa kwenye Uwanja wa Bouake mjini Bouake.
0 COMMENTS:
Post a Comment