Christiano Ronaldo ameweka rekodi mpya
ya ufungaji hat trick baada ya kufunga mabao matano wakati Real Madrid
ikiichapa Granada kwa mabao 9-1.
Ronaldo alifanikiwa kufunga mabao
matatu ndani ya dakika nane katika mchezo huo.
Pamoja na hivyo, Ronaldo atakuwa na
furaha zaidi baada ya kufanikiwa kumpita mpinzani wake Lionel Messi kwa mabao
manne.
Kwa mabao hayo matano, Ronaldo
amefikisha mabao 36 na kumpita Messi mwenye 32.
Awali Messi alikuwa na mabao hayo 32,
akiwa anampita Ronaldo kwa bao moja tu.
Ushindani kati ya Mreno huyo wa Real
Madrid na Muargentina wa Barcelona imekuwa kubwa.
Baadaye Barcelona ilijiongezea pointi
tatu kwa kuifunga Celta Vigo kwa bao 1-0, lakini Messi hakuweza kutikisa nyavu.
0 COMMENTS:
Post a Comment