April 29, 2015

COUTINHO AKIWA NA MURO KWENYE UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE, LEO.
Kiungo Andrey ameunganishwa katika kikosi cha Yanga kilishopaa kwenda Tunisia kuwavaa Etoile du Sahel.

Coutinho alikuwa kati ya wachezaji wa kikosi cha Yanga waliokuwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam tayari kwa safari hiyo.

Raia huyo wa Brazil amekuwa akisumbuliwa na majeraha mfululizo hali iliyomfanya ashindwe kuichezea Yanga.

Lakini leo alionekana yuko fiti na Jerry Muro amesema kuwemo kwake katika kikosi maana yake yuko tayari kwa mapambanano.

Yanga inaondoka na ndege ya Emirates kupitia Dubai hadi Tunis, baadaye watasafiri hadi Sousse kwenda kuwavaa Etoile katika mechi ya pili ya Kombe la Shirikisho.


Mechi ya kwanza jijini Dar es Salaam, ilimalizika kwa sare ya mabao 1-1 na Yanga inatakiwa kushinda au sare ya kuanzia mabao 2-2.

2 COMMENTS:

  1. MUNGU YUKO PAMOJA NANYI,TUNAWAOMBEA.

    ReplyDelete
  2. MUNGU YU PAMOJA NANYI,TUNAWAOMBEA.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic