WACHEZAJI WA YANGA, COUTINHO, JERRY TEGETE NA MRISHO NGASSA WAKIWA KWENYE UWANJA WA NDEGE WA JNIA MUDA MFUPI KABLA YA KUONDOKA KWENDA TUNISIA. |
Yanga inaondoka na ndege ya Emirates kupitia
Dubai hadi Tunis, baadaye watasafiri hadi Sousse kwenda kuwavaa Etoile katika
mechi ya pili ya Kombe la Shirikisho.
Mechi ya kwanza jijini Dar es Salaam,
ilimalizika kwa sare ya mabao 1-1 na Yanga inatakiwa kushinda au sare ya
kuanzia mabao 2-2.
Wachezaji wa Yanga walionekana kuwa watulivu na
waliwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam
mapema kabisa.
NIZAR KHALFAN, MBUYU TWITE NA KELVIN YONDANI... |
“Wachezaji wako vizuri, tunaanza safari ndefu
ya kwenda Tunisia. Wanayanga na Watanzania wanaopenda maendeleo ya soka la nchi
yetu watuombee,” alisema Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Yanga,
Jerry Muro.
Mechi hiyo imepangwa kuchezwa Jumamosi ingawa
Waarabu hao walikuwa wakigeuzageuza.
MURO AKIWA NA SHERMAN |
WE CAN ONLY TRUST IN GOD FOR A MIRACLE.AMEN.
ReplyDelete