Unaweza kuona kama maajabu, Kamati ya Rufaa
ya TFF imekutana leo kukaa kusikiliza rufaa ya Dk Damas Ndumbaro, bila ya
kumtaarifu.
Taarifa za uhakika zimeeleza kamati hiyo
imekaa leo jijini Dar es Salaam kusikiliza rufaa ya Dk Ndumbaro kupingwa
kufungiwa kujihusisha na masuala ya soka kwa miaka mitano.
“Kweli tuko, tumekaa kwenye kamati na ukweli
nikieleza Dk Ndumaro hajaitwa na hajui lolote,” kilieleza chanzo kutoka ndani
ya kamati hiyo.
“Unajua kinachoonekana kama TFF hawakutaka
kamati ikae, huenda kuna shinikizo
ili kutenda haki. Hivyo umefanyika ujanja Dk Ndumbaro asiitwe.
“Hiki ni moja ya mambo ya ajabu kutokea
katika soka, nilipofika hapa na kugundua Dk Ndumbaro hajaitwa kwa kweli
imenisikitisha sana.”
SALEHJEMBE ilimtafuta Dk Ndumbaro ambaye
alisema amepata taarifa hizo kupitia kwa rafiki yake.
“Kwa kweli mimi bado naona haya ni maajabu
katika soka. Nashangazwa sana na kinachoendelea kutokea, nimepewa taarifa na
mtu, aliniuliza jana, nikamuambia hawawezi kukaa bila ya kujipa taarifa.
“Mimi ndiyo mlalamikaji, watakaaje bila ya
kuniambia, si lahisi. Leo mtu kaniambia ndiyo kwenye kikao wanasikiliza rufaa
yangu, hii ni ajabu kabisa.
“Kutoka ofisini kwangu na ofisini kwa katibu
wa TFF ni mwendo wa dakika tano. Lakini sijapewa taarifa kuwa na kikao cha
rufaa yangu.
“Sitaki kusema maneno mengi sana, lakini
kupitia hili wadau wa soka wataona namna kulivyo na mambo ya kushangaza ambayo
hayapaswi kuvumiliwa.
“Sina hofu, naendelea kusubiri kwa kuwa
sijui mfumo uliotumika,” alisema Ndumbaro ambaye ni daktari wa sheria.
0 COMMENTS:
Post a Comment