Kocha Mkuu wa Yanga, Hans vand der Pluijm
amesema tuzo ambazo wachezajiw ake wamepewa na uongozi wa Yanga FaceBook Family
ni sehemu kubwa ya kuinua morali.
Kundi hilo liliwatuza wachezaji wa Yanga jana
wakiwa mazoezini likionyesha kuthamini mchango wao.
Pluijm amesema tuzo hizo zinawasaidia wachezaji
kujua wanafanya kazi kwa ajili yao lakini kuna watu nyuma yao.
“Jambo zuri, kitu kizuri mambo yafuate utaratibu
na inasaidia kwa timu. Hivyo wachezaji wajitambue zaidi ya hapo kuwa kuna watu
nyuma yao,” alisema.
Pluijm ni kati ya waliopewa tuzo hiyo kutokana
na mchango wake katika kikosi hicho ambacho sasa kinaelekea kubeba ubingwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment