Kipigo cha mabao 3-0 dhidi
ya Simba kiliwafanya mashabiki wa Ndanda FC waishio jijini Dar es Salaam
washindwe kujizuia.
Mashabiki hao waliingia
kwenye vurugu kubwa dhidi ya baadhi ya viongozi wao baada ya kipigo hicho
kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Mmoja wa shabiki alimtwanga
ngumi kiongozi mara tu baada ya mechi hiyo na kusababisha vurugu kubwa.
Hata hivyo, baadhi ya
mashabiki na viongozi waliingiza na kupoza ugomvi huo.
0 COMMENTS:
Post a Comment