April 17, 2015


Wapinzani wa Yanga kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Etoile du Sahel wamewasili jijini Dar es Salaam wakiwa tayari kabisa kuivaa Yanga kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.


Kikosi hicho kimewasili na ndege ya Kampuni ya Nouvelair  BJ 4870 wakiwa na msafara wa watu 56.

Wakiwa kwenye uwanja wa ndege wachezaji wa kikosi hicho cha Tunisia walionekana wako tayari kuivaa Yanga, kesho.

Msafara wao uliongozwa na Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka la Tunisia (FTF), Krifa Jalel, akiwa na Rais wa Etoile du Sahel, Charefeddine Ridha, wachezaji 19, benchi la ufundi lenye watu 13, waandishi wa habari 12 na wanachama 10.

Taarifa zimeeleza Etoile itafikia katika Hoteli ya Ledger Plaza, zamani ikijulikana kwa jina la Bahari Beach eneo la Kunduchi, ambapo leo Ijumaa jioni inatarajiwa kufanya mazoezi katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.


Waamuzi wa mchezo huo ni Samwel Chirindiza, Arsenio Marenguka, Celio de Jesus Musabe, Jose Maria Bachide wote kutoka nchini Msumbuji na wanatarajiwa kuwasili leo mchana, huku kamisaa wa mchezo huo, Salah Ahmed Mohamed kutokea nchini Sudan akitarajiwa kuwasili leo jioni na wote walitarajiwa kufikia katika Hoteli ya Protea iliyopo Oysterbay.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic