April 17, 2015


Ile ishu ya mshambuliaji Luis Suarez kumpiga tobo mbili beki David Luiz inazidi kupata umaarufu.

Suarez alimpiga Luiz tobo mbili na kufunga mabao mawili wakati Barcelona ilipoitwanga PSG mabao 3-1 katika Ligi ya Mabingwa Ulaya mjini Paris.

Hata hivyo imegundulika, kuwa Suarez ndiyo mchezo wake, alishampiga tobo tena Luiz wakati akiwa Chelsea, yeye akiwa Liverpool.
Mbaya zaidi, mitandaoni, mashabiki wamemgeuza Luiz kuwa ule mnara wa Eiffel wa Paris, kuwa katikati uko wazi, unapitisha tu mpira. Dah!




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic