NGASSA&MSUVA... |
Kiungo wa
zamani wa Yanga, Edibily Jonas Lunyamila ameibuka na kuwapa mbinu za kuwaondoa
Etoile du Sahel ya Tunisia kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika kuwa
ni kuhakikisha kesho wanashinda kuanzia mabao matatu.
Lunyamila
amefunguka kuwa siku zote asili ya soka la Waarabu ni kucheza kwa tahadhari
kubwa na kujilinda ili wakusubirie kwao, hivyo kuwataka Mrisho Ngassa, Simon
Msuva wa Yanga na wenzao kuhakikisha wanapata ushindi mkubwa nyumbani.
Lunyamila amesema
Yanga wanatakiwa kutumia mwanya huo kujihakikishia wingi wa mabao kwa kile
anachoamini ugenini ni pagumu kutoka.
“Waarabu wanajulikana.
Wanapokuwa ugenini wanataka kupunguza idadi ya mabao, hivyo hucheza soka la
kujilinda zaidi- wanasaka sare tu ili wakusubirie kwao,” alisema winga huyo
aliyetikisa miaka ya 1990.
0 COMMENTS:
Post a Comment