Etoile du Sahel wameendelea
na mazoezi ya nguvu ili kuhakikisha wanaing’oa Yanga.
Lakini wamekuwa wakiendelea
kuwaalika wachezaji wakongwe na maarufu wa klabu hiyo kwa lengo la kuwahamasisha
vijana wao.
Uongozi wa klabu hiyo
umekuwa ukitumia njia ya kuwaalika wakongwe kama sehemu ya hamasa ili timu yao
iing’oe Yanga.
Mazoezi yamekuwa
yakiendelea katika uwanja mdogo wa Sousse, lengo ni kuishinda Yanga.
Katika mechi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho, timu hizo zilitoka sare ya mabao 1-1.
Mechi yao ya marudiano ni
keshokutwa Jumamosi, itapigwa kwenye Uwanja wa Olimpiki mjini Sousse.
0 COMMENTS:
Post a Comment