TAMBWE WAKATI AKIICHEZEA SIMBA... |
Kamati
ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imeiagiza
klabu ya Simba kumlipa mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe kitita cha dola
7,000 (Sh milioni 14).
Tambwe
alikuwa mchezaji wa Simba hadi alipoachwa wakati wa dirisha dogo, aliwasilisha
malalamiko dhidi ya Simba ya kutolipwa dola 7,000 za Marekani zilizotokana na
klabu hiyo kuvunja mkataba wake Desemba 15, 2014.
Uamuzi
wa kuvunja mkataba ulikuwa ni wa makubaliano ya pande zote ambapo Simba
ilitakiwa iwe imemlipa fedha hizo mlalamikaji kufikia Desemba 17, 2014.
Katibu
Mkuu wa Simba SC , Steven Ally alikiri klabu yake kudaiwa na mchezaji huyo na
kuwa wameshafanya mawasiliano na wakili wake aliyepo Ureno, Felix Majani na
kupanga utaratibu wa kulipa isipokuwa kinachosubiriwa ni kusaini hati ya
makubaliano ya malipo (Deed of Settlement).
Kamati
imesikitishwa na klabu ya Simba kushindwa kumlipa mchezaji huyo kama ilivyokuwa
katika makubaliano ya kuvunja mkataba yaliyofikiwa na pande zote mbili Desemba
15, 2014.
Klabu
ya Simba inatakiwa kumlipa Amissi Tambwe fedha hizo kwa awamu mbili. Awamu ya
kwanza ya dola 5,000 malipo yawe yamefanyika kufikia Aprili 30, 2015. Salio la
dola 2,000 ili kukamilisha jumla ya dola 7,000 liwe limelipwa kufikia Mei 10,
2015, uamuzi ambao upande wa Simba ulikubaliana nao.
0 COMMENTS:
Post a Comment