Na
Saleh Ally
JONAS
Gerrard Mkude, mmoja wa viungo kinda kabisa hapa nchini ambaye ameonyesha njia
kwamba anaweza
soka,
akijiendeleza anaweza kufanya vizuri zaidi. Ukimtazama anaitumikia Simba, utakubaliana
nami na wengi wameliona hilo.
Mkude
amefanikiwa kuwafunika wageni kama Pierre Kwizera ambaye kwa mtazamo wangu,
kamwe hakuwa mchezaji mbaya lakini ubora wa Mkude ulifanya Simba ione hana
lolote na ikakubali kumuachia kiungo huyo raia wa Burundi aende zake
anapopataka.
Watanzania
nikiwemo mimi, tumekuwa tukililia Mkude apewe nafasi. Nimekuwa nikikasirishwa
na makocha wa kigeni wanaoshindwa kumuamini.
Mmoja
wa makocha hao ni Mart Nooij, raia wa Uholanzi, ambaye ameendelea kuteua kikosi
chenye wakongwe rundo huku akijua Stars sasa haiko katika mashindano yoyote,
hivyo ni bora kujenga kikosi cha chipukizi ambao watakuwa msaada baada ya mwaka
mmoja ujao.
Kumtetea
Mkude ni kutetea jambo moja kubwa ambalo Mtanzania yeyote mzalendo anapaswa
kulifanya. Nalo ni kutetea taifa letu. Mkude ni kijana wa Kitanzania, pia
kuitetea nchi yetu iwe na timu bora na kuachana na makocha wageni wanaotaka
kutetea vibarua vyao bila ya kuangalia manufaa itakayopata Tanzania.
Wakati
ninamtetea Mkude, ndiyo wakati huohuo ambao ninamkosoa bila haya hata kidogo,
bila woga wala kuhofia lawama.
Tanzania
inaharibikiwa na vitu vingi kwa kuwa watu wanahofia kulaumiwa. Watu wanataka
kuonekana wazuri na waungwana sana katika jamii fulani, hata kama wanaona mambo
yanaharibika.
Najua
ukweli unauma, lakini leo nafikisha ujumbe sahihi ninaoamini utakwenda kwenye
mirija ya damu ya moyo wa Mkude na kupitiliza kwenye ubongo wake kwa ajili ya kutafakari.
Akiwa ‘fair’ atayafanyia kazi, akiwa si hivyo, atanuna, mwisho ataendelea
kuharibikiwa na mimi nitaendelea kudunda kama kawaida, sitakosa chochote.
Nimekuwa
nikishangazwa na tabia ya Mkude, mara kadhaa nikimkuta katika ‘kibaa’ kimoja
eneo la Kijitonyama akipombeka. Wakati mwingine muda mchache kabla ya kwenda
mazoezini au baada ya kutoka.
Nimekuwa
nikimpita katika eneo hilo akiwa ameegesha gari lake aina ya Toyota GX 110
ambalo alipewa na uongozi wa Simba baada ya kusaini mkataba mpya. Usisahau pia
alikomba Sh milioni 40. Baada ya mkataba wake mpya tuliwasifia Simba, kwamba
wanatoa changamoto ya vijana wa Kitanzania kutamani kuwa kama Mkude.
Lakini
sasa inaonekana tofauti kwa kuwa nimepewa hadithi nyingi za tabia za ulevi za
Mkude. Hadithi yake ya kutafutwa usiku na baadhi ya viongozi, wakamkuta baa
akiwa amelewa chakari. Akapelekwa Zanzibar huku akijitapikia.
Siku
kadhaa zilizopita, Dawati la Championi lilifikishiwa malalamiko kwamba Mkude
amekuwa akishinda mtaa fulani, pombe kwenda mbele, mabinti wakiwa pembeni.
Lengo
langu si kumkorofisha Mkude, ingawa akiamua hivyo pia si shida kwa kuwa
Watanzania wengi kukosolewa ni uadui. Nataka nimuambie kwa kasi ya mbwembwe na
kufanya mambo ya ulimbukeni anayokwenda nayo, haitachukua muda atapotea.
Vijana
wengi wanaitaka nafasi yake, sasa kuna mtu kama Abdi Banda ambaye anaonyesha
kabisa ana ‘njaa’ ya mafanikio. Kama Mkude anaendelea hivyo, siku chache zijazo
atapotea na mwisho atawaangushia lawama viongozi kwa kuwa tunajua huwa
wanaharibu, itakuwa si rahisi kuamini kiungo huyo ana matatizo.
Nimekuwa
nikifuatilia uchezaji wake kwa karibu sana. Mara kadhaa, nimeona mambo ambayo
hayaniridhishi na hasa upotezaji wa pasi na upungufu wa nguvu ukilinganisha na
ilivyozoeleka. Naamini hii inatokana na ukosefu wa muda wa kupumzika vya
kutosha, utulivu wa kuwaza kazi na pia malengo au matamanio ya kufanya vizuri
zaidi.
Kweli
Mkude ana kipaji, lakini pombe na kutofuata utaratibu wa soka linataka nini,
umewamaliza wengi na Mkude anaweza kuwa shahidi, sihitaji kuwataja majina kwa
kuwa tupo nao mitaani.
Lazima
Mkude abadilike, lazima ajue yeye si Mtanzania anayejua mpira kuliko wote. Kama
anatamani kuwa kama mchezaji fulani wa Ulaya, lazima ajue mwenzake anajituma na
anafuata vizuri misingi ya nini soka linataka.
Kama
Mkude anaona gari alilonalo sasa ndiyo bora na kali kuliko yote, anajidanganya.
Akijituma atapata mshahara au maslahi bora zaidi na itakuwa rahisi kupata gari
bomba zaidi ya alilonalo.
Hakuna
binadamu aliyewahi kujisifia pombe imemsaidia, labda kiwanda cha bia ambacho
kinaingiza faida baada ya mauzo lakini si mtumiaji, kila mmoja analia na hasara
tu au majuto mwishoni!
Lazima
iwe sasa, huu ujumbe naufikisha kwako Mkude, ukibadilika, mambo yatakuwa poa na
itaonekana, uking’ang’ania mlango wa maisha uliyoingia, utaona kitakachofuata,
nacho ni aibu na utageuka mtu wa kulalamika tu.
SOURCE:
CHAMPIONI








Mkude if this is true you need to change this habit and think BIG. Look at Samatta his income is far away from yours ila sijawahi kusikia Sama amekutwa bar na mijimama amelewa na anajitapikia. Huu ni wakati wako kuhangaika kutafuta trial mbalimbali ikiwezekana hata kwa kujipeleka pasipo kusubiri waje.
ReplyDeleteAcha kaka utapotea mapemaaaa. Inatia huzuni sana wachezaji kuishia maisha ya kuchangiwa matibabu yenu wakati mnazo fulsa nyingi za kujiongezea vipato. Yawezekana ongezeko la kipato limekuja ghafla na hukuwa umejiandaa nalo; kama vipi ni heri utumie hilo ongezeko kufungua biashara mbalimbali au ukishindwa nenda katoe kwa YATIMA bro na Mungu atakubariki sana.
Nani kama Christopher Masawe Simba. Kiwango chake bado hujakifikia bro...Bonge la middle la ajabu...ila Mungu amrehemu na RIP Masawe ila mwisho wake wewe unaujua.
Ila tuna kina Mohamed Mwameja, Zamoyoni Mogella na wengine ambao maisha yao baada ya kuacha Soka wamejikita kwenye biashara na life inasonga mbele.
Mkude nikukumbushe ukianza kupata majeraha makubwa tu kwenye football ndio basi tena na Simba au timu yoyote inayokuona kama mfalme leo shughuli yake itakuwa imekwisha. Jipange Mkude haya maisha na huijui kesho yako wala huna miadi na Mungu aliyekuumba.
Ni ushauri tu
Mkude if this is true you need to change this habit and think BIG. Look at Samatta his income is far away from yours ila sijawahi kusikia Sama amekutwa bar na mijimama amelewa na anajitapikia. Huu ni wakati wako kuhangaika kutafuta trial mbalimbali ikiwezekana hata kwa kujipeleka pasipo kusubiri waje.
ReplyDeleteAcha kaka utapotea mapemaaaa. Inatia huzuni sana wachezaji kuishia maisha ya kuchangiwa matibabu yenu wakati mnazo fulsa nyingi za kujiongezea vipato. Yawezekana ongezeko la kipato limekuja ghafla na hukuwa umejiandaa nalo; kama vipi ni heri utumie hilo ongezeko kufungua biashara mbalimbali au ukishindwa nenda katoe kwa YATIMA bro na Mungu atakubariki sana.
Nani kama Christopher Masawe Simba. Kiwango chake bado hujakifikia bro...Bonge la middle la ajabu...ila Mungu amrehemu na RIP Masawe ila mwisho wake wewe unaujua.
Ila tuna kina Mohamed Mwameja, Zamoyoni Mogella na wengine ambao maisha yao baada ya kuacha Soka wamejikita kwenye biashara na life inasonga mbele.
Mkude nikukumbushe ukianza kupata majeraha makubwa tu kwenye football ndio basi tena na Simba au timu yoyote inayokuona kama mfalme leo shughuli yake itakuwa imekwisha. Jipange Mkude haya maisha na huijui kesho yako wala huna miadi na Mungu aliyekuumba.
Ni ushauri tu
Mkude anaelekea kuwa kama wachezaji wengi wa Kitanzania waliopoteza thamani ya vipaji vyao kwa kutojitambua, ni kweli asipokuwa makini atapotea mapema sana na hicho anachokipata leo hakitakuwa na msaada wowote kwa maisha yake, kikubwa Mkude na wachezaji wengine wanatakiwa kujitambua ya kuwa wao ni akina na nani na wanatakiwa kufanya nini. Labda nichukue nafasi hii kuwakumbusha viongozi wa hizi club zetu za hapa nchini wajaribu kuangalia uwezekano wa kuwa na mshauri katika timu labda inaweza kusaidia kwa wachezaji wetu kuwekwa sawa. Nilishawahi kusikia ya kuwa club za wenzetu huko nje zina watu wa namna hii ambao wameweza kuasaidia sana kwa timu kupata matokeo mazuri pindi wanapoongea na wachezaji kabla ya mechi na vilevile wameweza kusaidia kulinda viwango vya wachezaji. kitu nilichogundua wachezaji wengi wa Kitanzania bado hawajajua kuwa mchezaji wa Kimataifa nn unatakiwa kufanya wanaweza kujua ya unatakiwa kucheza kwa juhudi kubwa lakini bado hawajajua ni jinsi gani unaweza kulinda kiwango chako kwa muda mrefu.
ReplyDeleteNi ushauri tu kwa vilabu vyetu vya hapa nchini, tafadhali jaribuni kuangalia uwezekano wa kuwa na watu kama washauri kwa wachezaji nina imani wanaweza kusaidia..