WATANZANIA wameaswa
kuendelea kushiriki katika shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Kituo cha
Radio cha E FM kwa lengo la kuwasaidia kutimiza ndoto zao za maisha ya baadae
pamoja na kuliletea Taifa maendeleo.
Ushauri huo umetolewa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi
Mtendaji wa E FM, FRANCIS SIZA wakati wa hafla ya kutimiza mwaka mmoja tangu
kuanza kwa shughuli za urushaji wa matangazo ya Efm Radio.
Hafla hiyo imehudhuriwa na wageni mbalimbali akiwemo Meya wa
Manispaa ya Kinondoni YUSUPH MWENDA, Mbunge wa Kigoma Kusini Mheshimiwa DAVID
KAFULILA, Mheshimiwa ZITTO KABWE na Mkurugenzi wa Masoko kutoka Zantel,
SUKHWINDER BAJWA.
Katika hafla hiyo SIZA amesema kuwa ni muda muafaka sasa kwa
Watanzania kubadili maisha yao kuwa chanya kupitia E FM na kuahidi kuendelea
kutoa ushirikiano, kwani E FM ipo kw aajili ya Watanzania.
Wakati huohuo,Mstahiki
Meya wa MANISPAA ya Kinondoni YUSUPH MWENDA amesema kuwa, mbali na Efm kutoa
Burudani pia imetoa mchango mkubwa kutatua changamoto kwa wananchi.
MWENDA amewasihi wananchi hususani wa Kinondoni kutumia vyema
matangazo ya Efm Radio ili iwe rahisi kutatua kero mbalimbali.
Naye Mbunge wa Kigoma Kusini Mheshimiwa DAVID KAFULILA
amesema kuwa, ameguswa kwa kiasi kikubwa na vipindi mbalimbali vinavyoendeshwa
na Kituo hiki kwa kuwa vinaligusa Taifa.
Akimzungumzia kumkumbuka ZITTO KABWE akiwa ni rafiki yake
Bungeni na ni mmoja ya Wabunge wanaotoka wote mkoani wa Kigoma, Mheshimiwa KAFULILA amesema kuwa ,ZITTO
alikuwa ni miongoni mwa Wabunge vijana walioleta mabadiliko makubwa ya Kisiasa
nchini.
Kwa upande wake Mheshimiwa ZITTO KABWE amesema, kwa kipindi
kifupi, EFM imeonesha Taswira ya
hali ya juu inayoakisi hali halisi ya chombo cha habari kinavyotakiwa kuwa.
ZITTO amesema kuwa kwa kipindi cha mwaka mmoja kituo hiki
kimeonesha utofauti na Vyombo vya Habari vingine kwa kuwa kinajali sauti za
Wanyonge na si watu wenye nyadhifa Fulani katika jamii.







0 COMMENTS:
Post a Comment