Beki wa Simba, Abdi Banda
anashikiliwa na Jeshi la Polisi Tanzania kwa tuhuma za kushiriki upotevu wa
gari lililoibiwa.
Habari za uhakika
zilizoifikia SALEHJEMBE zimeeleza kuwa Banda anashikiliwa pamoja na mdogo wake
kwa tuhuma za wizi wa gari linalomilikiwa na mwanamke mmoja aliyeelezwa kuwa ni
mpenziwe.
Ingawa viongozi wa Simba
wamekuwa wagumu kupatikana na kuzungumzia suala hilo, lakini SALEHJEMBE
imethibitisha Banda ameshikiliwa kituoni hapo tokea jana usiku.
Mmoja wa askari wa kituo
cha Magomeni amethibitishwa kushikiliwa kwa beki huyo mwenye uwezo wa kucheza
kama kiungo na uchunguzi unaendelea.
“Kweli yuko kituoni
anashikiliwa, anashikiliwa yeye na mdogo wake kuhusiana na kuibiwa kwa gari la
dada mmoja anayeelezwa ni mpenzi wa mchezaji huyo,” alisema.
Taarifa zinaeleza Banda
amekuwa akilianzima gari hilo na kulitumia kila mara.
“Kweli amekuwa akilitumia
gari hilo lakini yeye hajui kuendesha. Mdogo wake amekuwa akiendesha gari hilo
na kuna mkanganyiko wa taarifa.
“Inaelezwa wakati
linapotea yeye alikuwa jijini Mbeya Simba ilipokwenda kuivaa Mbeya City. Lakini
mmiliki wa gari anasisitiza Banda ndiye alilianzima kupitia mdogo wake. Hivyo
tumewaachia polisi wafanye kazi yao,” alieleza ndugu wa Banda.
Viongozi wa Simba
walikuwa hawapokei simu zao lakini ilielezwa Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Stephen
Ally alikuwa katika kituo hicho cha Magomeni akilishughulikia suala hilo.
0 COMMENTS:
Post a Comment