Kiungo wa Yanga, Simon
Msuva amezidi kupaa katika upachikaji mabao katika Ligi Kuu Bara baada ya
kufunga mabao mawili leo na kufikisha 16.
Msuva amezidi kujichimbia
kileleni katika nafasi ya ufungaji bora lakini bao alilofunga kwa kichwa cha
kuchupa katika mechi dhidi ya Ruvu Shooting ndiyo limekuwa gumzo zaidi.
Bao hilo limekuwa
likifafanishwa na lile alilofunga mshambuliaji Robin van Persie wa Man United
wakati akiitumikia timu yake ya taifa ya Uholanzi wakati wa Kombe la Dunia
nchini Brazil, mwaka jana.
Msuva naye alichupa
kuiwahi krosi safi ya Haruna Niyonzima na kupachika bao hilo.
Baada ya hapo mashabiki
wamekuwa wakijadili kwenye mitandao mbalimbali wakijaribu kulilinganisha bao
hilo na lile la van Persie.
Anayemfuatia Msuva kwa
wingi wa mabao ni Amissi Tambwe ambaye amefunga bao moja leo na kufikisha 11.
Hivyo kufanya wachezaji
hao wawili wa Yanga kumpiku Didier Kavumbagu wa Azam FC mwenye mabao 10 ambayo
yalimfanya aongoze kwa muda mrefu.
Mwingine mwenye mabao 10
ni Emmanuel Okwi aliyepachika Hat Trick katika mechi yao ya mwisho dhidi ya
Mgambo Shooting, juzi.
0 COMMENTS:
Post a Comment