DK NDUMBARO AKIWA MAKAO MAKUU YA FIFA KATIKA JIJI LA ZURICH NCHINI USWISS. |
Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF) limeamua kuweka wazi msimamo wake wa kuhakikisha Dk
Damas Daniel Ndumbaro haokoki katika kifungo cha miaka 7 alichofungiwa
kujishughulisha na masuala ya soka.
Awali,
TFF ilikuwa ikituhumiwa kumfungia Dk Ndumbaro kwa woga kwamba ni tishio kwa
uongozi wa TFF.
Juzi
ikatuhumiwa kufanya njama ashindwe kutokea katika kikao wakati rufaa yake
ikisikilizwa na Katibu Mkuu, Mwesigwa Celestine akazungumzia hilo huku akisema
kuwa taarifa ya yeye kwenda kwenye kikao ilipaswa kutolewa na Mwenyekiti wa
Kamati ya Rufaa, jambo ambalo pia lilipingwa na Dk Ndumbaro.
Lakini
leo, TFF rasmi imeweka pingamizi kupinga kusikilizwa kwa rufaa ya Dk Ndumbaro. Taarifa kutoka ndani ya kamati hiyo ya rufaa zimeeleza TFF inapinga kusikilizwa kwa rufaa ya mwanasheria huyo maarufu, kitu kinachoashiria inataka adhabu yake iendelee.
Tayari
Dk Ndumbaro alishailipa TFF kitita cha Sh milioni moja ili rufaa yake
isikilizwe.
Sasa
TFF iliyomfungia, TFF iliyopokea fedha zake ili rufaa isikilizwe ndiyo
inayopinga tena rufaa isisikilizwe.
Juhudi
za kumpata Dk Ndumbaro alizungumzie suala hilo zinaendelea na juhudi za
kuwapata TFF nao zinaendelea.
Mbona wewe unamshabikia sana Ndumbaro una maslahi gani kwake?
ReplyDelete