Kiungo mwenye kasi wa Yanga, Mrisho Ngassa ameonyesha yeye kuwa ni kijana mwenye vipaji vingi.
Ngassa ameonyesha ana uwezo wa kudaka kwa kukaa langoni na kuzuia michomo kama ambavyo yeye amekuwa akiwateza makipa.
Alifanya hivyo katika mazoezi ya Yanga kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar. Kiungo huyo alikuwa akiwatania makipa Ally Mustapha 'Barthez' na Deo Munishi 'Dida' kwamba atawapa upinzani mkubwa katika namba hiyo ya mlinda lango.
Yanga iko katika maandalizi kwa ajili ya mechi ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Etoile du Sahel ya Tunisia, Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
0 COMMENTS:
Post a Comment