MSUVA AKIKABIDHIWA TUZO. |
Mashabiki na wanachama wa
Yanga tawi la Kitunda jijini Dar es Salaam, walionyesha uzalendo kwa klabu yao
baada ya kutoa tuzo kwa baadhi ya wachezaji wa kikosi cha Yanga.
Walitoa tuzo kwa baadhi ya
wachezaji wakiwemo Ally Mustapha 'Barthez', Haruna Niyonzima, Simon Msuva na Nadir Haroub ‘Cannavaro’.
Lengo la wanachama na
mashabiki hao ni kuonyesha kuunga mkono juhudi za kikosi hicho. Tawi hilo changa lililofunguliwa Aprili 19 limeonyesha mfano na kati ya waliokabidhi tuzo hizo ni Hashim Abdul ambaye ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya tawi hilo la Kitunda.
Tuzo hizo zilikabidhiwa
mara tu baada ya mechi ya Stand United ambayo Yanga ilishinda kwa mabao 3-2 na
kubakiza pointi sita tu ili itangazwe kuwa bingwa.
NIYONZIMA AKIPOKEA TUZO. |
NAHODHA CANNAVARO NAYE ALIPEWA TUZO |
0 COMMENTS:
Post a Comment