KESSY AKIPAMBANA NA AZIZ GILLA WA MGAMBO... |
Beki wa kulia wa Simba, Hassan Kessy ndiye kiboko kwa upigaji wa krosi katika Ligi Kuu Tanzania Bara.
Kessy alipiga krosi 18 katika mechi moja wakati Simba ilipopambana na Mgambo Shooting na kushinda kwa mabao 4-0 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, jana.
Kessy aliyejiunga na Simba akitokea Mtibw Sugar, pamoja na kufanya ulinzi kwa uhakika huku akimthibiti vilivyo Aziz Gilla, alikuwa akipanda na kupiuga krosi hizo safi.
Beki wa kushoto wa Simba, Mohammed Hussein 'Tshabalala' naye anaonekana wamo kwani alipiga krosi 11 katika mechi hiyo.
Beki Juma Abdul, licha ya timu yake kucheza katika kiwango cha chini katika mechi dhidi ya Stand United alifanikiwa kupiga krosi 12 huku Oscar Joshua akipiga krosi 7 katika mechi hiyo ambayo Yanga ilishinda kwa mabao 3-2.
Waandishi mnatuharibia mpira wetu!! Hivi ligi kuu ni simba na yanga tu!!? Unaweza kuniambia Yanga na Coast zilipigwa kross ngapi!!? Nyie ndo mnawavimbisha vichwa wachezaji wetu wakati uwezo ni mdogo
ReplyDeleteSifa zisizozaa hazina faida.
ReplyDelete