Makamu wa Rais wa klabu hiyo, Geofrey Nyange
‘Kaburu’ alijikuta akilazimika kufanya kazi ya ziada kusaidia kumbembeleza
kiungo Jonas Mkude katika msiba wa baba yake mzazi.
Mkude alikuwa ni mtu mwenye uchungu,
alishindwa kujizuia na kulia kwa nguvu hali iliyomfanya Kaburu amsogelee na
kuanza kuzungumza naye akimshawishi kuwa mvumilivu.
Hata hivyo, Mkude alishindwa kujizuia na
kuzidi kulia akionyesha kuhuzunisha watu wengi pale msibani.
Kuona hivyo, Kaburu alichukua uamuzi wa
kumkumbatia na kumueleza maneno kadhaa ambayo angalau yalionyesha kumtuliza.
Baba yake alifariki juzi na kumlazimisha
Mkude kuondoka kambini Simba mjini Shinyanga kurejea jijini Dar.
Maziko yamefanyika katika makaburi ya
Kinondoni jijini Dar es Salaam.
0 COMMENTS:
Post a Comment