GARCIA AKIFANYIWA MAHOJIANO NA WAANDISHI JIJINI DAR ES SALAAM, LEO. |
Mshambuliaji hatari wa zamani wa Barcelona
na Liverpool, Luis Garcia amesema wanataka ushindi katika mechi dhidi ya nyota
wa Tanzania kwenye Uwanja wa Taifa, Jumamosi.
AKIZUNGUMZA NA 'BONGE' SALEH ALLY... |
Garcia amesema kikosi cha wakongwe wa
Barcelona kina wachezaji wengi bora ingawa wanajua utakuwa mchezo mgumu.
Akizungumza na SALEHJEMBE jijini Dar es
Salaam, Garcia amesema yeye na baadhi ya wachezaji wameishawasili jijini Dar.
“Tutakuwa hapa Tanzania tukisubiri mchezo
huo, tumeambiwa kwamba kikosi cha Watanzania ni kizuri.
“Hivyo tumeijiandaa na tunajua haitakuwa
kazi lahisi lakini tunachotaka ni ushindi,” alisema.
Garcia aliwahi kuichezea Barcelona katika
kikosi kimoja na Ronaldinho.
Wachezaji wengine watakaokuwa katika kikosi
kitakachocheza Jumamosi ni pamoja na Mandieta, Patrick Kluivert, Deco na
wengine ambao imeelezwa watatajwa baadaye.
0 COMMENTS:
Post a Comment