Kiungo mshambuliaji, Haruna
Moshi ‘Boban’ na kipa, Juma Kaseja ni kati ya wachezaji watakaoiongoza timu ya
Dar City kesho Jumapili kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Kombaini ya Vikawe
iliyopo Pwani.
Kwa mujibu wa mratibu wa
mechi hiyo, Athuman Tippo ‘Zizzou’, mchezo umeandaliwa maalum kwa ajili ya kuhamasisha
michezo mkoani Pwani.
SALEH ALLY (KULIA) AKIPAMBANA KATIKA MOJA YA MECHI.... |
Tippo alisema kikosi cha
Dar City kitajumuisha pia baadhi ya Waandishi wa Habari za Michezo akiwemo
Saleh Ally na Wilbert Molandi wa magazeti ya Championi na watangazaji Shaffih
Dauda na Mbwiga Mbwiguke wa Clouds Media Group.
Alisema mechi hiyo
inatarajiwa kuchezwa Jumapili saa 10:00 kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Vikawe
uliopo Kibaha.
“Kikubwa tunataka
kuhamasisha michezo huko Vikawe na katika kutimiza hilo, tumepanga kucheza
mchezo mmoja wa kirafiki na wakazi wa huko kwa kuwatumia wachezaji, waandishi
na watangazaji maarufu nchini,” alisema Tippo.
0 COMMENTS:
Post a Comment