Mambo magumu. Straika Said Bahanuzi wa Polisi Moro, amesema kuna kazi
ngumu ya kuinusuru timu yake isishuke daraja msimu huu.
Polisi Moro inayomilikiwa
na Polisi, inashika nafasi ya 12 katika msimamo wa timu 14 za Ligi Kuu Bara
ikiwa na pointi 25 baada ya kucheza mechi 24 za ligi hiyo.
Bahanuzi anayecheza kwa
mkopo katika timu hiyo akitokea Yanga, alisema: “Inaniuma kuona timu yangu ipo
mkiani na kuna hali ya hatari ya kushuka daraja, tunahitaji kujituma ili
kuibakiza timu katika ligi.”
“Kuna kazi kubwa ya kufanya
kuhakikisha timu inabaki katika ligi, hasa kwa kushirikiana na wachezaji
wenzangu, vinginevyo aibu itatukuta.”
Hivi karibuni kocha Amri
Said alijiondoa kuifundisha timu hiyo ambayo awali ilimtimua Adolf Rishard,
hivyo sasa ipo chini ya John Tamba.
0 COMMENTS:
Post a Comment