Beki kinda wa Simba, Hassan Kessy ameonyesha ni muungwana baada ya kuwaomba radhi makocha na wachezaji wenzake kutokana na kitendo chake cha kususia kambi.
Kessy alisusia kambi kwa madai ya kutolipwa fedha zake za usajili Sh milioni 5 pamoja na nyumba ya kuishi.
Tayari uongozi wa Simba umemkabidhi Kessy fedha kwa ajili ya nyumba na hadi ya kumalizia fedha zake za usajili.
Kessy ambaye ameenguliwa katika kikosi cha Simba kilichokwenda Mbeya kwa ajili ya kuivaa Mbeya City kwa kuwa hakuwa pamoja na wenzake wakati wa maandalizi.
Hata kabla ya kuenguliwa Kessy alijumuika mazoezi na wenzake katika Viwanja vya Chuo Kikuu Dar es Salaam.
Akiwa mazoezini alizungumza na wenzake na kuwaomba radhi, hali kadhalika makocha. Kwamba haikuwa sahihi, lakini sasa amejifunza na wamsamehe.
Kessy alipotafutwa kuhusiana na hilo, alisema: “Kweli nimerejea na kujiunga na wenzangu, wakirudi nitaungana nao tena.
“Lakini nisingependa kulizungumzia zaidi suala hilo, kikubwa ni kuwa nimerejea kuitumikia Simba kwa kushirikiana na wenzangu,” alisisitiza beki huyo aliyejiunga na Simba akitokea Mtibwa Sugar wakati wa dirisha dogo la usajili.
0 COMMENTS:
Post a Comment