Etoile du Sahel wametua nchini wakiwa
tayari, usidhani hawajajiandaa kwa kuwa tayari wachezaji wawili raia wa Algeria
wameandaliwa kuimaliza Yanga.
Washambuliaji hao wawili raia wa Algeria
ambao Baghdad Bounedjah na Kaddour
Beldilali ndiyo wanaonekana kupewa jukumu la kubaki mbele kuimaliza Yanga.
Etoile kutoka Tunisia imepanga kujilinda
sana katika mechi yake ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Yanga jijini Dar es
Salaam, kesho.
Pamoja na Waalgeria hao, wachezaji wengine
wa kigeni ambao ni Franck Kom (Cameroon) na Alkhali Bangoura (Guinea).
Bangoura amekuwa akisifika kwa kupiga
mashuti lakini Waalgeria hao wawili ndiyo mtambo wa mabao wa kikosi hicho cha
Etoile.
Baghadad pia ana kasi, mjanja na mwepesi
kupiga mashuti ya kushitukiza. Mabeki wa Yanga lazima wawe makini.
Ukiachana na wachezaji hao wanne, wachezaji
wengine 14 waliobaki katika kikosi hicho ni raia wa Tunisia.
Yanga imeendelea kujifua vikali kujiandaa na
mechi yake dhidi ya Etoile du Sahel ya Tunisia.
0 COMMENTS:
Post a Comment