April 6, 2015


Mtibwa Sugar wamekiri kwamba kweli sasa maji ya shingo na lazima wafanye juhudi kuhakikisha hawaporomoki hadi daraja la kwanza.


Mtibwa sasa watu wamekuwa 'wakijipigia' tu na leo imekamilisha mchezo wake mwingine ambao imepoteza dhidi ya Stand United ilipolala kwa bao 1-0.

Msemaji wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amekiri kuwa hali yao si nzuri kama ambavyo wamekuwa wakiona na kusema wanalazimika kupambana.

"Kwa kweli lazima tukubali hali si nzuri, mwendo ni mbaya. Utaona hapo Shinyanga tumepoteza mechi mbili mfululizo.
"Tumefungwa na Kagera halafu Stand. Tunakiri hali si nzuri kabisa na hata sisi tumekuwa tukijiuliza ni nini cha kufanya.
"Inatuchanganya, lazima tukiri kwamba inatuweka katika wakati mgumu lakini lazima tupambane," alise,a Kifaru.

Mtibwa Sugar ilimaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara bila kupoteza hata mechi moja.

Ndiyo ilikuwa timu iliyokuwa kileleni huku Simba, Yanga na Azam FC zikiifukuza. Lakini sasa ni kati ya zile zinazopambana kuhakikisha haziteremki daraja.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic