Yanga wamesema wanatoa shukurani zao kwa Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia ambaye alisafiri na timu hiyo hadi nchini Zimbabwe.
Mkuu wa kitengo cha habari cha Yanga, Jerry Muro amesema Nkamia ambaye ni mbunge wa Kondoa Kusini alishirikiana nao bega kwa bega.
"Tunawashukuru wote walioshirikiana nasi wakiamini Yanga ilikuwa ikipambana kwa ajili ya Wanayanga na pia taifa," alisema Muro.
"Mheshimiwa Nkamia ni kati ya watu tunaowashukuru sana, kwani licha ya kwamba alikuwa kuwa kiongozi wa Simba lakini alipambana vilivyo pamoja nasi."
Nkamia ambaye kitaaluma ni mwanahabari, aliwahi kufanya kazi TBC pamoja na mashirika mengine mbalimbali ya kimataifa kama BBC.
Yanga ilikuwa nchini Zimbabwe kuivaa FC Platnum ya Zimbabwe katika mechi ya Kombe la Shirikisho na kuvuka kwa jumla ya mabao 5-2.
Sasa Yanga itakutana na Etoile du Sahel ya Tunisia katika mechi inayotarajiwa kuwa ngumu sana.
0 COMMENTS:
Post a Comment