AMRI SAID |
Baada ya Polisi Morogoro
kukubali kipigo cha mabao 4-0 kutoka kwa maafande wenzao wa Mgambo JKT, kocha
wa timu hiyo, Amri Said ‘Jaap Stam’, amewatupia lawama mabeki wake kwa kusema kuwa
ndiyo waliosababisha kichapo hicho.
Mgambo wakiwa kwenye uwanja
wao wa nyumbani, Mkwakwani, waliweza kuishushia Polisi Moro kipigo hicho, kwa
mabao ya Full Maganga, Salum Gilla na Malimi Busungu aliyepiga mawili.
“Timu ilicheza vizuri ila mabeki ndiyo walichangia kwa
asilimia kubwa tupoteze mchezo huu, wamefanya makosa mengi ya kizembe ambayo
wapinzani wetu wameyatumia kutufunga, kama wangekuwa makini tusingepoteza
mchezo huu,” alisema Amri Said, mchezaji wa zamani wa Simba.
0 COMMENTS:
Post a Comment