Kocha Mkuu wa Yanga,
Mdachi, Hans van Der Pluijm, amefunguka na kuelezea sababu ambazo zitamfanya
kuwamaliza mapema Waarabu wa Tunisia, Etoile du Sahel, katika michuano ya Kombe
la Shirikisho Afrika.
Yanga ni kama imetupwa
kwenye kundi la siafu kwa kukutanishwa na mabingwa hao wa zamani wa Kombe la
Shirikisho katika raundi wa pili, ambapo mshindi ataingia hatua ya makundi.
Pluijm amesema anajua ‘nature’
ya soka la timu kutoka Tunisia kuwa zinacheza soka la akili, nidhamu, kiufundi
zaidi na kubwa kuliko ni soka la kukaba kila idara.
Katika hilo, Pluijm alisisitiza
kuwa wanatakiwa kutumia zaidi faida ya nyumbani kujiwekea akiba ya mabao,
vinginevyo wanaweza kujikuta pabaya.
“Kikubwa tunahitaji kuwa
makini, kucheza kitimu zaidi, tukipata mabao yetu ni lazima safu ya ulinzi iwe
makini kwa kujipanga zaidi, maana unajua kinachofuata unapokuwa kwenye ardhi
yao,” alisema na kuongeza kuwa pia anahitaji kupata CD zao ili kuwajua
nje-ndani.
“Moja ya kazi zangu ni
kuhakikisha napata data za kutosha kuhusiana nao ili tujipange zaidi, nadhani
itasaidia kwa kiasi kikubwa, ingawa tunahitaji maandalizi ya kutosha kama kila
kitu tutakifanya kwa umakini, hakika tutawatupa nje.”
0 COMMENTS:
Post a Comment