Kikosi cha Yanga
kitakachoivaa Coastal Union kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, leo kitamkosa
kiungo wake mwenye kasi, Mrisho Ngassa, ambaye anasumbuliwa na nyama za paja.
Ngassa alikuwa miongoni mwa
nyota waliokosa mazoezi ya jana asubuhi kwenye Uwanja wa Karume, Dar
wakijiandaa na mchezo dhidi ya Coastal Union.
Wengine ambao walifika
mazoezini lakini hawakujumuika katika mazoezi ya jumla ni Said Juma Makapu na
Danny Mrwanda ambaye alikuwa anasumbuliwa na tumbo.
Kocha Mkuu wa Yanga, Hans
van Der Pluijm, amesema kuwa Ngassa hataweza kucheza leo.
“Ngassa atapumzika,
anasumbuliwa na nyama za paja, hivyo nimemwambia apumzike. Kama ameshindwa
kufanya mazoezi na wenzake, maana yake hawezi kucheza mchezo wa kesho (leo) dhidi ya Coastal Union,” alisema
Pluijm.
0 COMMENTS:
Post a Comment