Kikosi cha wakongwe wa Barcelona kimeibuka na
ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya nyota wakongwe wa Tanzania katika mechi ya kirafiki iliyopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Mshambuliaji Patrick Kluivert ndiye alikuwa
shujaa baada ya kufunga mkwaju wa penalti wa bao la pili.
Kluivert alifunga mkwaju huo na kumuacha kipa
Juma Kaseja akianguka kushoto kwake na mpira ukiingia kulia.
Barcelona walikuwa wa kwanza kufunga bao kupitia
kwa Luis Garcia ambaye aliwachambua mabeki wa Tanzania wakongwe na kufunga.
Yusuf Macho ‘Musso’ akafunga baso safi la pili
kwa shuti kali katika dakika ya 42. Mabao hayo yalidumu hadi mapumziko.
Barcelona ndiyo walikosa nafasi nyingi zaidi za
kufunga kupitia kwa Garcia na Gaizka Mandieta ambaye alicheza beki wa kulia.
Idadi ya watu uwajani hapo haikuwa kubwa sana na
ilielezwa kutokana na tatizo la kutokuwa na matangazo au taarifa ya kutosha
kuhusiana na mechi hiyo na wengine walilalama kuhusiana na kiingilio.
0 COMMENTS:
Post a Comment