MSOLLA (KUSHOTO) AKIWA NA RAIS JAKAYA KIKWETE. |
Siku kadhaa baada ya Taifa Stars kupangwa
Kundi G na Nigeria, Misri na Chad katika kuwania kufuzu Kombe la Afrika 2017, kocha
wa zamani wa timu hiyo, Mshindo Msolla amesema kikosi hicho hakitafuzu kwani
mwalimu wake anapoteza muda tu nchini.
Msolla ambaye ndiye kocha wa mwisho
kuifundisha Taifa Stars kabla ya ujio wa Marcio Maximo mwaka 2006, aliliambia
Championi Jumamosi kuwa, Tanzania haitafanya vizuri kwani kocha wake Mart Nooij
hana mtazamo wa kimaendeleo na soka la nchi hii.
Alisema Nooij hajafanya jambo lolote la msingi
kuhakikisha Taifa Stars inapiga hatua, badala yake anasubiri mkataba wake uishe
aondoke.
“Hatutafanya
lolote mbele ya mataifa kwa sababu ya kocha wetu wa sasa wa Taifa Stars, hana mtazamo
wa kimaendeleo wa soka la nchi hii,” alisema Msolla.
“Tangu amefika hakuna alichokifanya cha maana
kwa ajili ya timu na soka la Tanzania, badala yake anaangalia mshahara wake mzuri
na kulinda CV yake isichafuke tu.”
Taifa Stars itaanza na Misri kati ya Juni 12
na 14, mwaka huu kufuzu Kombe la Afrika 2017.
0 COMMENTS:
Post a Comment