April 29, 2015



Kocha wa Simba, Goran Kopunovic amesema maandalizi ya kikosi chake yanampa jibu kuwa watapambana hadi mwisho katika mechi yao dhidi ya Azam FC.



Kopunovic raia wa Serbia amesema kama hawawatakuwa na majeruhi, basi kikosi chao hakitayumba.

"Katika ligi ya Tanzania, hauwezi kuidharau timu yoyote. Tunachoangalia ni kufanya vizuri na tunajua mechi dhidi ya Azam FC itakuwa na upinzani mkubwa.

"Wanaitaka nafasi ya pili kama sisi, lakini kila timu inataka pointi tatu ndiyo maana nasisitiza ushindani utakuwa mkubwa sana," alisema Kopunovic.

"Nimezungumza na wachezaji, kwamba tunachotakiwa ni kushinda. Wao wanajiandaa vipi, sisi si kazi yetu, tupambane kushinda tu," alisisitiza.

Simba inatarajia kukipiga na Azam FC wikiendi hii ikiwa ni mbio za kuwania nafasi ya pili kwa kuwa bingwa tayari amejulikana ambaye ni Yanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic