April 24, 2015



MPIRA UMEKWISHA:
Muda mwingi Yanga wanaonekana kumiliki mpira huku wakiwa wameridhika na mabao waliyopata. JKT wanajitahidi kushambulia lakini hawako makini.
Dk 74, Mtindi anapata nafasi nzuri lakini anapiga shuti buuuuuuuu
Dk 70 Ally Mtindi anaingia ndani ya eneo la boksi na kupiga shuti lakini Barthez anaokoa

GOOOOOOO Dk 67 Sherman anafunga bao la tano kwa kichwa akiiwahi krosi ya nzuri ya Abdul Juma

KADI Dk 64, Yahaya Tumbo na Kelvin Yondani wanalambwa kadi ya njano. Hata hivyo Tumbo ndiye aliyempiga Yondani ngumi

GOOOOOOOOO Dk 58, Tambwe anaifungua Yanga bao la nne baada ya mabeki wa Ruvu kujichanganya na yeye anamalizia kwa ufundi mkubwa. Hilo ni bao lake la 11

Dk 56 Ngassa anapata nafasi nyingine lakini anashindwa kufunga, kipa anadaka
Dk 50, Ngassa anapiga shuti kali kwa mguu wa kulia lakini mpira unagonga mtambaa wa panya na kuokolewa
Dk 46, Yanga wanaanza mpira kwa kasi lakini Ruvu nao wanajibu mashambulizi kwa kasi kubwa

MAPUMZIKO
GOOOOOOO Dk 45, Msuva anafunga bao la tatu, la pili kwake leo na la 16 kwake msimu huu

Dk 36, Msuva anapoteza nafasi nyingine tena baada ya shuti lake kupaaa
Dk 31, Abrahman Mussa anapiga shuti, linatoka nje kidogo ya lango la Yanga.
KADI Dk 27 Beki George Michael Osei analambwa kadi ya njano kwa kumpiga pepsi Ngassa tena kwa makusudi kabisa

 GOOOOOOOOO Dk 23, Sherman anaunganisha vizuri na kuifungia Yanga bao la pili likiwa lake tatu msimu huu

Dk 21, Joshua anapiga shuti kali baada ya Yanga kushambulia lakini kipa Rashid anadaka kiufundi kabisa
Dk 15&18 Yanga ndiyo wanaoonekana kushambulia mfululizo lakini Ruvu wanakuwa makini kuokoa
GOOOOOOOO Dk 13 Msuva anaifungia Yanga bao kwa kichwa baada ya kuunganisha krosi safi ya Niyonzima
Dk 12, Ruvu wanafanya kosa tena, lakini Tambwe anashindwa kuuwahi mpira, unaokolewa
Dk 10, Msuva tena anapata nafasi lakini anashindwa kuuwahi mpira
Dk 7, Msuva anapoteza nafasi nzuri kabisa baada ya kuiwahi krosi nzuri ya Oscar Joshua, lakini yeye na kipa, anashindwa kufunga.


Mechi imeanza kwa kasi, Yanga ndiyo wanaoshambulia zaidi huku wakiwa wamepiga mashuti mawili yaliyolenga lango huku Ruvu wakiwa wamefanikiwa mara moja na kupiga krosi nzuri lakini ikaokolewa.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic