Ratiba ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa
Ulaya imetangazwa leo baada ya droo kufanyika.
Mabingwa watetezi Real Madrid wamepangiwa
kukipiga na Juventus wakati utamu zaidi uko katika mechi ya pili ambayo
inawakutanisha Barcelona dhidi ya Bayern Munich.
Mechi ya Madrid inaonekana kutokuwa gumzo
zaidi kwa kuwa Juventus haipewi nafasi sana.
Lakini Barcelona na Bayern ndiyo gumzo na
kila mmoja anataka kujua nani nakwenda fainali.
Mechi mbili za mwanzo za nusu fainali
zitapigwa Mei 5 na 6 na timu hizo zitarudiana Mei 12 na 13.
0 COMMENTS:
Post a Comment