April 22, 2015


MPIRA UMEKWISHAAAA.....
DAKIKA 4 ZA NYONGEZA
Dk 84&89 zaidi mpira unachezwa katikati ya uwanja na wachezaji wanacheza katika tahadhari kubwa kutokana na maji mengi uwanjani

KADI Dk 83 Mwamuzi anamlamba Juuko kadi ya njano kwa kumfanyia Busungu faulo ya makusudi. Ilikuwa faulo mbaya, angeweza hata kulambwa kadi nyekundu

Dk 77, Simba wanamtoa Jonas Mkude, nafasi yake inachukuliwa na William Gallas

Dk 76 Mgambo wanamtoa Mohammed Samatta, nafasi yake inachukuliwa na Ayoub Saleh
Dk 74, Simba wanaamka tena, Okwi anawatoka mabeki watatu wa Mgambo na kutoa pasi nzuri kwa Mkude ambaye anapiga shuti kali kipa anadaka, linamtoka lakini anauwahi tena mpira

Dk 69&73 Mgambo wanaonekana kubadilika na sasa ndiyo wanaotawala mpira. Wamefika langoni mwa Simba mara nne lakini bado hawajafanikiwa kufunga bao

Dk 67, Maganga anapoteza nafasi nzuri ya kufunga akiwa katika nafasi nzuri, hatua nne kutoka katika lango la Simba

Dk 66, Simba wanamuingiza Issa Rashid kuchukua nafasi ya Ajibu

KADI Dk 65 Ajibu analambwa kadi ya njano ya kijinga kabisa, alipiga mpira huku akiwa ameishasikia filimbi
Dk 60, Simba wanamtoa Singano na kumuingiza Simon Sserunkuma

Dk 58 Ivo Mapunda anafanya kazi nyingine nzuri kwa kuokoa shuti kali na kuwa kona, lakini Mgambo wanashinda kuitumia kupata bao

Dk 54 mvua kubwa inaporomoka na kusababisha kidogo SImba kupunguza kasi ya mashambulizi.
GOOOOOOOOO Dk 51 Okwi anaifungia Simba bao la nne baada ya kuwachambua kama karanga mabeki wa Mgambo na kuuachia mpira uende wavuni

Dk 50, Okwi tena anaingia ndani ya eneo la hatari la Mgambo, anapiga mpira unaopita juu kidogo ya lango la Mgambo
DK 46, Simba inaanza kwa kushambulia kwa kasi kubwa, inapata kona lakini haina matunda baada ya Singano kupaisha kwa kupiga shuti kuubwaa akiwa katika nafasi nzuri

MAPUMZIKO
DAKIKA NNE ZA NYONGEZA
Dk 45, Ajibu anampiga chenga kipa, huku beki mmoja akiwa langoni, anashindwa kufunga mwenyewe...goal kick

Dk 42, Aziz Gilla akiwa amebaki na lango anashindwa kufunga kwa kupiga shuti kali linalopaa

GOOOOOO Dk 41 Okwi tena anaifungia Simba bao la tatu baada ya mabeki Mgambo kujichanganya na yeye kumtoka mmoja wao kabla ya kufunga kwa shuti kali.  Dk 39, Singano anapiga shuti, mabeki Mgambo wanaokoa na kuwa kona isiyo na faida kwa Simba
KADI: Dk 35 Fully Maganga analambwa kadi ya njano SUB: Dk 31 Abuu Daudi Anatoka anaingia Hahim Chanacha kwa upande wa Mgambo


Dk 26, Ivo Mapunda anafanya kazi ya ziada kumkimbiza mshambuliaji wa Mgambo, anautoa mpira na kuwa kona isiyozaa matunda

Dk 25, nafasi nyingine kwa Simba lakini Awadhi Juma anapaisha juuu
Dk 23, Okwi anawatoka mabeki Mgambo na kupiga krosi nzuri, wanaokoa na kuwa kona isiyokuwa na matunda

Dk 19, Simba wanafanya shambulizi jingine, krosi safi ya Kessy lakini kipa Mgambo anaokoa
GOOOOOO Dk 15, Singano 'Messi' anaifungia Simba bao la pili kwa mkwaju wa adhabu, inajaa moja kwa moja wavuni

Dk 12, Okwi anawatoka mabeki wa Mgambo lakini anaangushwa na mwamuzi anasema ipigwe faulo 
Dk 10, Okwi akiwa amebaki yeye na lango, anapiga mpira unatoka nje

GOOOOOO Dk 8, Okwi anaifungia SImba bao la kwanza baada ya kuunganisha krosi safi ya Kesssy aliyegongeana Singano.
DK 5, Tayari Mgambo wamepata kona mbili na Simba kona moja na timu zinaendelea kushambuliana kwa zamu.

Mgambo ndiyo wanaanza kwa kushambulia zaidi, ndani ya dakika mbili za kwanza wako kwenye lango Simba.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic