SHOE KUSHOTO, AKIPAMBANA NA ZINEDINE ZIDANE WAKATI AKIICHEZEA BAFANA BAFANA. |
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi
ametuma salamu za rambirambi kwa Rais wa Chama cha Mpira wa Miguu cha Afrika
Kusini (SAFA) Dr.Danny Jordan kufuatia kifo cha nguli aliyewahi kuichezea timu
ya Taifa ya nchi hiyo (BafanaBafana) John Lesiba "Shoe" Mashoeu
kilichotokea jana Aprili 21.
Katika salamau zake kwa Dk Jordan, Malinzi amesema nchi ya
Afrika Kusini imepatwa na pigo kubwa katika tasnia ya mpira wa miguu, kufuatia
kifo cha Mashoeu aliyefariki dunia kwa ugonjwa wa Kansa ya Utumbo, na
kusema watanzania wako nao pamoja katika kipindi hiki cha maombelezo.
John Lesiba "Shoe" Mashoeu aliyezaliwa Disemba
18, 1965 nchini Afrika Kusini, alikuwa ni miongoni wa wachezaji wa nchi hiyo
waliotwaa Ubingwa wa Kombe la Mataifa Afrika (AFCON) mwaka 1996 nchini Afrika
Kusini na baadae kushiriki fainali za Kombe la Dunia nchini Ufaransa mwaka
1998.
Wakati wa uhai wake Mashoe alipata kuvichezea vilabu vya Giant
Blackpool, Kaizer Chiefs, Amazulu na Alexandria United vya Afrika Kusini, na
timu Gencleribirligi, Kocaeilispor, Fenerbahce na Busrsapor za Uturuki.
0 COMMENTS:
Post a Comment