Mkoani Arusha mwishoni mwa juma hili kunataraji kufanyika
michuano ya NDONDO CUP itakayoshirikisha jumla ya timu nane kutoka mkoani hapa.
Lengo la michuano hiyo ni kuwakutanisha wapenda soka mkoa wa
Arusha pamoja na kuwapa nafasi wa mashabiki wa mchezo huo Mkoani
hapa kukutana sehemu moja.
Michuano hii itaanza kutimua vumbi siku ya Ijumaa ya tarehe
24/04/2015 na kufika tamati siku ya jumapili.
Mshindi wa kwanza katika michuano hii atapata zawadi ya fedha
taslimu shilingi laki tano (500,000) pamoja na kikombe, mshindi wa pili
atajipatia fedha taslimu shilingi laki tatu (300,000).
Timu zitakazoshiriki katika michuano ya NDONDO CUP 2015 ni FFU
OLJORO, TANZANITE SPORTS FOUNDATION, RED STAR, TANZANITE VETERAN, LEMARA BOYS,
NJIRO SPORTS, SMALL NYOTA na UMBRELA GARDEN.
Ratiba katikIMA MICHUANO HIYO NI KAMA IFUATAVYO
FFU OLJORO VS TANZANITE SPORTS CLUB, TANZANITE VETERAN VS RED
STAR, LEMARA BOYS VS UMBRELA GARDEN, NJIRO SPORTS VS SMALL NYOTA
Michezo yote itapigwa siku ya ijumaa kwa mfumo wa bonanza na
nusu fainali itakuwa siku ya jumamosi wakati mchezo ya fainali utapigwa siku ya
jumapili.
Michuano hii itafanyika katika uwanja wa AICC uliopo karibu na
round about ya KIJENGE. muda ni kuanzia saa 4 asubuhi mpaka 12 jioni.
0 COMMENTS:
Post a Comment