Siku chache
tangu aliyekuwa kocha wa muda wa Polisi Morogoro, Amri Said atangaze kubwaga
manyanga kuifundisha timu hiyo, imebainika kuwa Yanga ndiyo chanzo.
Amri anadaiwa
kufanya hivyo kutokana na kuhofia kipigo kutoka kwa Yanga kama ilichokumbana
nacho Coastal Union ya Tanga cha mabao 8-0, kwa kuwa Yanga inatarajiwa kucheza
na Polisi Moro hivi karibuni.
Amri alisema
kukosa ushirikiano klabuni hapo ni sababu kubwa ya kujiondoa huku ikizingatiwa
kuwa timu hiyo ipo katika nafasi mbaya kwenye Ligi Kuu Bara.
“Kila
nililokuwa nikiwaambia waliona ni jambo la kawaida wakati timu ipo kwenye
nafasi mbaya, nikaona ni bora nijiondoe kuliko kuja kuharibu CV yangu na ukizingatia
timu hiyo bado hajacheza na Yanga, yasije kunikuta kama yaliyomkuta ndugu yangu
Julio (Jamhuri Kihwelo, kocha wa Coastal),” alisema Amri.
Hahahahahahahahaha,jamani Yanga mnatisha!
ReplyDelete