Licha ya mshambuliaji wa
Yanga, Mliberia, Kpah Sherman, kufunga mabao mawili tu kwenye ligi, ameanza
kupata jeuri na kusema kuwa kwa sasa amebadilika na hataki mchezo uwanjani,
atakuwa na kazi moja tu ya kuhakikisha anafunga mabao katika kila mechi.
Sherman ambaye alitua Yanga
katikati ya msimu huu, akitokea timu ya Centikaya ya nchini Cyprus, alitajwa
kuwa mfumania nyavu hatari, lakini haikuwa hivyo kwenye mechi zote alizocheza
kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara.
Lakini kwenye mechi mbili
zilizopita ameibuka ghafla na kufunga bao kwenye ushindi wa mabao 8-0, walioupata
dhidi ya Coastal Union na kisha kwenye ushindi wa 3-1 mbele ya Mbeya City.
Sherman alisema, alikuwa akiteseka sana pale alipoona hafungi mabao,
lakini kwa sasa ameshapata dawa, ndiyo maana kwenye mechi mbili zilizopita
ameweza kufunga bao katika kila mechi na hataishia hapo.
Alisema alikuwa
akisumbuliwa na aina ya uchezaji wa Yanga, lakini dawa inayomfanya abadilike ni
kuwa sasa ameshajua namna ya kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kufunga mabao
kirahisi.
“Sasa ni muda wangu wa
kufunga, nimejiuliza sana kwa nini nilikuwa sifungi, lakini nimeshapata jibu,
ndiyo maana unaona nafunga, sitaishia hapa nasema huu ndiyo mwanzo, nitazidi
kuifungia Yanga katika kila mechi nitakayocheza” alisema Sherman.
Yote yanawezekana, hata kama hafungi ila jamaa anajua sana maana anatoa assist za ukweli
ReplyDelete