Kiungo
tegemeo wa Yanga, Salum Telela, bado haijabainika kama atarejea hivi karibuni
uwanjani kutokana na majeraha aliyonayo, lakini habari njema kwa Wanayanga ni
kwamba kiungo wao, Andrey Coutinho amerejea uwanjani.
Telela
aliumia kifundo cha mguu na kushindwa kumalizia mechi wikiendi iliyopita
walipokuwa wanaumana na Mbeya City kwenye Uwanja wa Taifa ambapo Yanga
ilishinda 3-1.
Daktari
wa Yanga, Juma Sufiani, amefafanua kuwa, tayari ameshamfanyia matibabu Telela
ingawa bado ana maumivu ambayo bado hayajatoa picha halisi kama ataweza kurejea
hivi karibuni au la.
“Telela
tumemfanyia vipimo, kifundo cha mguu ndiyo kinamsumbua lakini ni mapema mno
kusema sasa atakaa nje baada ya muda gani kulingana na maumivu aliyonayo,”
alisema Sufiani.
Kwa upande wa Coutinho amesema:“Kwa sasa nipo fiti kabisa kuweza
kurejea uwanjani na kuendelea kucheza kama ilivyokuwa hapo awali na nimejipanga
vya kutosha kuhakikisha napambania namba yangu katika kikosi cha kwanza.
“Najua itakuwa siyo rahisi kutokana
na viwango ambavyo vinaonyeshwa na wachezaji waliopo kama Msuva na Ngassa
lakini nitampambana mpaka mwisho.”
0 COMMENTS:
Post a Comment